Barua ya Katibu Mkuu Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. V.T Wonanji imetoa idhini ya kupandisha hadhi Zahanati ya Likombe na Mikindani zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuwa vituo vya afya.
Idhini ya kupandishwa hadi vituo imetolea Machi 24,2020 baada ya ya Wizara hiyo kupitia taarifa ya ukaguzikutoka katika kamati ya usimamizi wa huduma za afya za Mkoa na kuridhia kwa vituo hivyo kupandishwa hadhi.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Likombe Nuru Namkuna amesema kuwa kupandishwa hadhi kwa zahanati hizo na kuwa vituo vya afya kuna faida kubwa ikiwemo kuongeza mapato ya kituo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.