Jumla ya miradi 7 ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 8,694,076,0967 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru 2019 ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko Oktoba 7,2019 wakati akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara QS. Omari Kipanga katika viwanja vya Mirumba vilivyopo Kata ya Jangwani
Akitoa mchanganuo wa fedha hizo Mwaigobeko amesema kuwa katika fedha hizo shilingi milioni 7,650,000 ni mchango wa Wananchi, Milioni…………… mchango wa halmashauri , Serikali kuu ni ……….. na wahisani wamechangia shilingi bilioni………...
Ukiwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwenge wa Uhuru umezindua mradi mmoja wa Ujenzi wa visima vitatu vya mkono Mkundi, Umefungua miradi mitatu ya Ujenzi wa Nyumba mbili za Wakuu wa Idara, Ujenzi wa kiwanda kidogo cha Wajasiriamali pamoja na Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari ya Bandari
Aidha Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la Msingi Mradi wa Zahanati ya Mbawalachini pamoja na kuona na kukagua miradi miwili ya ujenzi wa soko la kisasa Chuno pamoja na ujenzi wa mfereji wa kuondoa maji ya Mvua kutoka Nabwada hadi Mtepwezi.
Mwenge wa Uhuru 2019 ulipokelewa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Oktoba 7,2019 na kukimbizwa kwa KM 57.7 katika Kata saba kati ya Kata kumi na nane zilizopo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.