Pichani ni kikundi cha Usafi cha Mtwara Kuchele wakiwa wameshika kadi zao za Bima afya mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa
Kikundi cha usafi cha akina mama kinachojulikana kwa jina la Mtwara Kuchele ambacho kimekuwa kikifanya usafi kuzunguka maeneo mbalimali ndani ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani kimepatiwa kadi za Bima ya afya ishirini na mbili bure zenye thamani ya shilingi 600,000 ikiwa ni moja wapo ya kutambua mchango mkubwa wanaouofanya ndani ya Manispaa yetu.
Kadi hizo ambazo zimetolewa na Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kutumia mapato ya ndani zitawasaidia akina mama hao kupata huduma bure katika Zah anati ,Vituo vya afya na hospitali ya rufaa ikiwamo wao wenyewe pamoja na familia zao na hivyo kuwa na uhakika wa afya zao.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi kadi hizo iliyofanyika Januari 12,2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa ametoa kadi hizo ili kuwafanya akina mama kufanya kazi zao vizuri.
“Afya ni jambo la msingi ili watu waweze kufanya uzalishaji, shughuli za kiuchumi wanapaswa kuwa na afya ambayo inawawezesha kufanya shughuli zao vizuri Zaidi na ivyo kukuza uchumi binafsi na Kitaifa” alisema Mwaigobeko.
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. geofrey Mwanichisye amewapongeza akina mama hao kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa kuwa Seriakli ina Imani kubwa na kikundi hiko na ndio maana wamepewa kadi za bima ya afya.
Aidha amewata akina mama hao kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano kwa kulipa kodi lakini pia kuwahimiza wananchi wengine kulipa kodi kwa Maendeleo ya Manispaa na Taifa kwa ujumla.
Kadi za Bima ya afya zilizotolewa zilikabidhiwa kwa kikundi hiko na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod MManda aliyewasilisha ombi la kikundi hiko kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.