MTWARA-MIKINDANI YAGAWA VIFAA VYA USAFI VYA MIL.12.7
Katika kuhakikisha kuwa Mji wa Mtwara unakuwa safi muda wote Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupitia Mradi wa uendelezaji Mji MKakati (TSCP) imekabidhi vifaa vya usafi vyenye thamani ya shilingi Milioni 12,700,000 kwa vikundi kumi na mbili vya Usafi na kwa watumishi wanaofanya kazi katika dampo la Mangamba.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Oktoba 7,2020 katika eneo la Dampo kuu la Mangamba Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa na timu yake kwa kuwawezesha vikundi hivyo na kuwarahisishia utendaji wao wa kazi.
Aidha Kyobya amevitaka vikundi hivyo kutunza vitendea kazi walivyokabidhiwa na kuvisimamia ili viweze kudumu kwa muda mrefu lakini pia amewataka kuvifanyia kazi iliyokusudiwa.
Kwa upande wake Hamza Masudi Licheta Mwenyekiti wa kikundi cha Usafi kwanza ameishuku Manispaa kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani imewaondolea uhaba wa vifaa waliokuwa nao
“Kwanza tuishukuru Manispaa kwa jambo jema lililofanya ,tulikuwa tunapata shida kw akuwa vifaa vilikuwa vichache, ni matuini yetu yangu kuwa kwa sasa suala lamusafi kwneye masoko na maneo mengine yatakwenda vuziri”alisema Licheta.
Vikundi vilivyopata vifaa ni Pamoja na kikundi cha Mtwara Kuchele, Usafi kwanza, ndoa wasiwasi, Manispaa Group, Wakukaya Chuno, Ligula C, Saba Saba, Reli Gropu, Umoja Group, Nalendele Group Pamoja na Kikundi cha Jamii.
Kwa upande wa Vifaa vilivyokabidhiwa ni Pamoja na Matololi, “Gum boot”, fyekeo, Fagio, ‘Gloves’, Makasha ya kutunzia taka, Sepetu, ‘Over roll’, Mashine ya kufyekea, Mipira ya kumwagilia maji Pamoja na Safety Boot’
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.