Kupitia Mradi wa uendelezaji Miji Mkakati (TSCP) Manispaa ya Mtwara-Mikindani imesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 na Kampuni ya SEURECA International ya nchini ya Ufaransa.
Mkataba huo uliosainiwa Mei 10,2019 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ukishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara na wataalamu umelenga kufanya usanifu wa kuondoa maji ya mvua
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara. Mhe Evod Mmanda ameishukuru Serikali kwa kutengeneza miundombinu ya maji safi na maji taka katika Mji wa Mtwara akiamini kuwa baada ya mradi huo kukamilika Manispaa itakuwa nzuri na tatizo la mafuriko litaisha.
Amewataka wakandarasi kufanya kazi kwa muda uliopangwa na kwamba ana Imani kuwa tatizo la mafuriko katika mji wa Mtwara linaenda kuisha. Aidha amewataka kushirikisha wananchi katika zoezi zima la ukusanyaji wa taarifa ili miundombinu inayoka kujengwa ilingane na mazingira yaliyopo.
Akiongea kwa upande wa Kampuni ya SEURECA Kiongozi wa mradi huo Dkt. Dimitries Etraimidis amesema kuwa katika ufanikishaji wa kazi hiyo anategemea kupata ushirikiano wa kutosha kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa na kuahidi kuwa kazi waliyopewa wataifanya kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Col. Emanuel Mwaigobeko ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuwezesha mradi huu utakaosaidia kutatua tatizo la mafuriko katika Mji wa Mtwara aidha amewashukuru TAMISEMI kwa usimamizi wa miradi na msaada mkubwa wanaotoa katika ofisi yake.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.