Katika kuhakikisha kuwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu vinaimarika kiuchumi Manispaa ya Mtwara-Mikindani imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 224,194 kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Walemavu.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mikopo hiyo iliyofanyika Juni 21,2019 katika ukumbi wa benki kuu, bwana Yasini Saidi aliyemuwailisha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ameipongeza Manispaa kwa kutii agizo la Serikali la kutenga asilimia 10 kutoka mapato ya ndani kuwezesha wanawake, Vijana na walemavu.
Amesema kuwa lengo la Serikali kutoa mikopo kwa makundi hayo ni kuhakikisha inawainua wajasiriamali kutoka katika hatua moja ya maendeleo kwenda hatua nyingine na ndio maana imeamua kutoa riba katika mikopo hiyo.
Pamoja na hayo Yasini amewataka wajasiriamali kuwa makini na kuhakikisha kuwa malengo yao yanatimia kwa kutumia mkopo huo kwa malengo yaliyokusudiwa.
‘Niwaombe huu mkopo mlioupata leo mkautumie kulingana na mpango wa kikundi chenu ili muweze kurejesha kwa wakati na wenzenu waweze kukopeshwa.” alisema Yasini.
Nae Naibu Meya wa Manispaa Bi. Shadida Ndile amewaasa wanavikundi hao kutumia mkopo kwa maendeleo na kuwataka wanawake kutokubali kurubuniwa na waume zao kwa kuwapatia fedha hizo hali itakayopelekea kutorejesha fedha kwa wakati. Pia amewataka kutotumia fedha hizo kurejesha madeni ya kwenye vikoba.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya huduma za Jamii mhe Hassani Namkami amesema kuwa mikopo inayotolewa na Manispaa haiangalii itikadi za dini, siasa wala kabila hivyo kila mmoja ana haki ya kupata mkopo ili mradi awe amekidhi vigezo.
Akiongea kwa niaba ya vijana wenzake Abillahi Ally Katibu kikundi cha Muungano ameushukuru uongozi wa Manispaa kwa kuwapatia mkopo na kuahidi kufanya kazi kwa bidi ili waweze kurejesha kwa wakati. Aidha ametoa wito kwa vijana wenzake wafanye kazi na kuacha kukaa vijiweni kwa kuw fursa za mikopo zipo.
Awali akisoma taarifa ya mikopo MKuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii bi Juliana Manyama amesema kuwa Manispaa ilipokea maombi ya mkopo kutoka vikundi 42 vya wajasiriamali wenye thamani ya shilingi milioni 293,983,100.
Amesema kuwa baada ya kupitia maombi hayo vikundi vyote 42 vilikidhi vigezo na kupatiwa mkopo wa milioni 224,154,000 kwa vikundi 40 vya wanawake (216,354,000 ), kikundi 1 cha vijana (3,800,000) na kikundi 1 cha walemavu(4,000,000).
Ameongeza kuwa pamoja na mkopo uliotolewa leo tayari Manispaa ilishatoa mkopo wa milioni 9,926,000 kwa vikundi 3 vya walemavu mapema mwezi Novemba mwaka jana na kufanya fedha iliyokopeshwa kwa vikundi hadi 1sasa kufikia milioni 225,080,000.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.