Kutokana na kufanya vizuri kwenye matumizi, ukusanyaji wa mapato na utekelezaji mzuri wa Miradi ya Maendeleo kulikopelekea Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ametoa pongezi kwa Manispaa hiyo.
Byakanwa ametoa pongezi hizo kwenye baraza maalumu la Madiwani la kupitia taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali za mwaka 2018/2019 lililoketi May 14,2020 katika Ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari ya call and Vision.
Pamoja na pongezi hizo byakanwa pia amemtaka Mkurugenzi na timu yake kuhakikisha kuwa wanazuia kutokea kwa hoja za ukaguzi mwisho wa siku hati safi ipatikane bila ya kuwa na hoja kabisa na kuhakiksha hoja zilizobaki zinafungwa
Aidha ameitaka manispaa hiyo kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za uhaba wa madarasa, matundu ya vyoo Pamoja na changamoto zingine.
“Msingi mkubwa, kiini, roho ya halmashauri ni mapato kwa hiyo niwaombe muongeze nguvu za kuweza kusimamia na kudhibiti vyanzo vya mapato ya ndani na vilevile kufata utaratibu wa matumizi ya fedha zinazokusanywa na kuletwa na Serikali kuu, Alisema Byakanwa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko katika taarifa yake amesema kuwa halmashauri kwa mwaka wa 2018/2019 ilipokea hoja 25, zilizofungwa ni hoja saba na kubakiwa na hoja 18 amzabo zinaendelea kufanyiwa kazi.
Awali akisoma taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali za mwaka 2018/2019, Mwakilishi wa Mkaguzi Mkuu wa hesabu za nje Mkoa wa Mtwara Ibrahim Mdendemi ameipongeza Ofisi ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kupata hati safi.
Amesema kuw ripoti ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali yam waka 2018/2019 iliwasilishwa kwa mkurugenzi ikiwa na jumla ya hoja ishirini na tano , baada ya kupokea utekelezaji jumla ya hoja saba zimefungwa na hivyo kusalia na hoja 18 ambazo hazijafungwa saw ana asilimia 76.
Kuanzia mwaka 2015/2016 hadi sasa Manispaa ya Mtwara-Mikindani imekuwa ikipata hati safi kwa miaka minne mfululizo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.