Baraza la madiwani la Manispaa ya Mtwara-Mikindani limepitisha kwa aslimia mia moja rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 yenye jumla ya fedha kiasi cha shilingi yenye thamani ya shilingi bilioni 39,080,277,666 .
Akisoma taarifa ya mawasilisho ya mapendekezo hayo kwenye baraza la maalumu la madiwani la kupitia bajeti hiyo lililofanyika februari 7,2019 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa hiyo, Mchumi wa Manispaa bwana Mensaria Mrema amesema kuwa katika makadiro hayo Manispaa imelenga kukusanya shilingi bilioni 4.9 kutoka katika mapato ya ndani, ruzuku ya matumizi ya kwaida milioni 658,ruzuuku ya mishahara bilioni 16.8na miradi ya maendeleo bilioni 16.7
Amesema kuwa mpango huu wa bajeti umelenga katika kuboresha maeneo mbalimbali ndani ya Manispaa kwa kuangalia vipaumbele vilivyogusa sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya na ustawi wa jamii, Maji na udhibiti wa maji taka, kilimo, mifugo na uvuvi, Majengo na miundombinu, Ardhi, misitu na maliasili, Maendeleo ya jamii, Utawala, Fedha na biashara.
Katika sekta ya elimu Manispaa imepanga kuboresha miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari ikiwemo ujenzi wa madarasa, kujenga nyumba za walimu ,kujenga matundu ya vyoo, kuongeza udahili wa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza ,ununuzi wa vifaa vya kufundishia, kuboresha mlo wa mchana kwa wanafunzi, kuongeza idadi ya walimu pamoja na kununua vifaa vya maabara.
Kwa upande wa sekta ya afya Mrema amesema kuwa Manispaa imelenga kupunguza vifo vya akina mama na Watoto pamoja na kuimarisha huduma na upatikanaji wa vifaa tiba kwa kuboresha miundombnu ya afya kwa kujenga zahanati mbili, kuimarisha upatikanaji wa vifaa tiba ,kusimamia matumizi ya mfumo wa Gothomis, kununua dawa na vitendanishi pamoja na kutenga shilingi 1000 kwa kila mtoto kwa ajili ya lishe.
Sekta ya Maendeleo ya jamii manispaa imelenga kuwezesha wananchi kiuchumi kwa kutenga asilimia 10 katika mapato ya ndani kuwezesha vikundi vya wanawake,Vijana na walemavu, kutenga maeneo ya wajasiriamali na viwanda na upande wa utawala manispaa imelenga kuimarisha usalama ndani ya manispaa na kuboresha mazingira ya watumishi ya kufanyia kazi.
Sekta nyingine ni fedha na biashara ambapo manispaa imepanga kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kutoka 4.8 bilioni hadi 4.9 bilioni kwa kuongeza mashine za kukusanyia mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato na kwa upande wa kilimo,mifugo na uvuvi manispaa imelenga kudhibiti uvuvi haramu ,kuongeza kasi ya uzalishaji mazao ya chakula na biashara, kuongeza thamani ya mazao pamoja na kuimarisha vyama vya ushirika.
Pamoja na hayo Mrema ameongeza kuwa katika kupanga bajeti hiyo manispaa imezingatia vigezo mbalimbali vikiwemo Mpango mkakati wa manispaa wa mwaka 2018/2019-2022/2023, wasifu wa halmashauri wa mwaka 2017, ilani ya uchaguzi ya Chama tawala ya mwaka 2015/2020, vipaumbele vya wananchi vilivyotokana na jitihada za jamii, sheria ya bajeti ya no. 11 ya 2015.
Vigezo vingine ni pamoja na mwongozo wa Serikali uliotolewa na wizara ya fedha mwaka 2018 juu ya maandalizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2010, Malengo endelevu ya maendeleo ya umoja wa mataifa ya mwaka 2016, Maagizo na ahadi za viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na mapitio ya mpango wa maendeleo wa mwaka 2018/2018.
Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 Manispaa ilipanga kukusanya fedha kaisi cha shilingi bilioni 29,144,145,260 kutoka katika vyanzo mbalimbali , kufikia Disemba 2018 Manispaa imeshakusanya fedha kiasi cha shilingi bilioni 14,123,869,490.51 (mapato ya ndani bilioni 1.368,584,953.70 sawa na asilimia 29), (Misharaha 6,379,030,000 sawa na asilima 44), (Matumizi mengineyo shilingi 338,622,427 sawa na asilimia 50), (Miradi ya Maendeleo 6,037,632,109.8 sawa na asilimia 134.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.