Manispaa ya mtwara –Mkindani tumepokea fedha shilingi 499,200,000 kutoka Serikali kuu (Tamisemi) kupitia program ya Lipa kulingana na matokeo (EP4R) zitakazo tumika kwenye ujenzi wa miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari.
Kwa upande wa shule za Msingi tumepokea 172,800,000 za ujenzi wa madarasa manane pamoja na matundu ya vyoo thelathini na sita.
Shule za Msingi zilizopata fedha ni Pamoja na Shule ya Msingi Mangowela imepokea 53,000,000 (ujenzi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo kumi na mbili), Mivinjeni 40,000,000 (ujenzi wa Madarasa mawili, Magomeni 13,200,000 (Ujenzi wa matundu ya vyoo kumi na mbili)
Shule ya Msingi Mbae 53,000,000 (Ujenzi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo kumi na mbili) pamoja na Shule ya Msingi Ufukoni 13,200,000 (ujenzi wa matundu ya vyoo kumi na mbili).
Kwa upande wa Sekondari tumepokea 326,400,000 za ujenzi wa madarasa manane, ukamailishaji wa nyumba ya mtumishi pamoja na ukamilishaji wa maabara kumi na nane.
Shule zilizopata fedha ni Pamoja na Shule ya Sekondari Mangamba imepokea 13,200,000 (ujenzi wa matundu ya vyoo kumi na mbili), Mikindani 10,000,000 (ukamilishaji wa nyumba nyumba moja ya mtumishi), Naliendele 40,000,000 (ujenzi wa madarasa mawili), Bandari 40,000,000 (ujenzi wa madarasa mawili).
Mitengo 40,000,000 (ujenzi wa madarasa mawili) Pamoja na Shule ya Sekondari Saba Saba 40,000,000 ( ujezi wa madarasa mawili).
Shule nyingine za Sekondari zilizopata fedha za ukamilishaji wa maabara ni Pamoja na Shule ya sekondariChuno, Rahaleo, Saba Saba , Shangani, Sino Tz na Sekondari ya Umoja kwa gharama ya shilingi 180,000,000 huku kila shule ikipata 30,000,000
Tayari fedha zimeshaingia kwenye akaunti za shule na utekelezaji wa ujenzi utaanza hivi karibuni mara baada ya taratibu za kutafuta mafundi zikikamilika.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.