Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko (aliyevaa sare za jeshi) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya mtwara QS.Omari kipanga
Umoja, Mshikamano, Uaminifu na Uadilifu vyaipeleka Manispaa ya Mtwara-Mikindani kushika nafasi ya tatu Kitaifa katika Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 kwa kupata alama 83.24.
Manispaa pia imeshika nafasi ya kwanza Kanda ya Kusini inayohusisha Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Katavi na Rukwa. Pia imeshika ya kwanza Kimkoa inayohusisha Halmashauri 9.
Tunaishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya kwa kutuongoza vema.
Pia tunawashukuru viongozi wa dini,Viongozi wa vyama vya siasa, waandishi wa habari, wadau mbalimbali wa Maendeleo pamoja na Wananchi wote wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kujumuika pamoja na sisi kuanzia kwenye utekelezaji wa miradi ya Maendeleo iliyopitiwa na Mwenge, Mapokezi ya Mwenge Mikindani hadi eneo la Mkesha tuendelee kushirikiana ili kuleta Maendeleo ya katika halmashauri yetu.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani ilipokea Mwenge wa Uhuru Oktoba 7,2019 na kukimbizwa kwenye miradi 7 yenye gharama ya shilingi Bilioni 8.6 na hakuna Mradi uliokataliwa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.