Kupitia Mpango wa Programu ya Lipa Kulingana na Matokea uliopo katika Sekta ya Elimu nchini(EP4R) Manispaa ya Mtwara-Mikindani imepokea shilingi 839,000,000 kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya shule (madarasa, mabweni,bwalo na vyoo) na ufuatiliaji katika Shule za Msingi nane na Sekondari nne.
Manispaa imepata fedha hizo ikiwa ni motisha baada ya kuzingatia viwango vya ufanisi na kukidhi vigezo (viashiria) kupitia miradi ya EP4R ya ukamilishaji wa maboma ya madarasa iliyotekelezwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Shule zilizopata fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo ni Pamoja na Shule za Msingi za Tandika shilingi 48,000,000 (madarasa mawili na matundu manane ya vyoo), Naliendele shilingi 66,600,000 (madarasa matatu na matundu sita ya vyoo), Mlimani shilingi 47,700,000 (madarasa mawili na matundu saba ya vyoo ), Mivinjeni shilingi 46,600,000 (madarasa mawili, matundu sita ya vyoo), Majengo shilingi 67,500,000 (madarasa 3, matundu matano ya vyoo), Lilungu shilingi 48,600,000 (madarasa 2, matundu sita ya vyoo), Kwale shilingi 67,500,000 (madarasa matatu na matundu matano ya vyoo) na Shule ya Msingi Chikongola shilingi 49,700,000 (Madarasa mawili na matundu saba ya vyoo).
Kwa upande wa Sekondari Shule ya Umoja imepata shilingi 42,000,000 (madarasa mawili), SabaSaba Shilingi 42,000,000(madarasa mawili), Naliendele 182,000,000 (ujenzi wa bweni la wanafunzi na bwalo la chakula) na Shule ya Sekondari Mikindani imepata shilingi 122,000,000( ujenzi wa madarasa mawili na bweni la wanafunzi).
Ujio wa fedha hizi kwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni faraja kwani itasaidia kupunguza changamoto za miundombinu ya madarasa, vyoo na mabweni tlakini itasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Hii si mara ya kwanza kwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupata fedha za EP4R mwaka wa fedha wa 2018/2019 ilipokea shilingi 275,000,000 za programu hii kutekeleza umaliziaji wa maboma ya madarasa 22 ya Shule za Msingi za Kwale,Tandika na Naliendele na shilingi 100,000,000 za umaliziaji wa maboma ya madarasa manane ya Shule za Sekondari za Mitengo,Mangamba , Sino na Shangani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.