Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bwana. Grayson Orcado akipokea Vitabu Vya Kujifunzia kutoka kwa Bi. Joyce Shuma Mwakilishi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania leo Januari 29,2020 katika Ofisi za Manispaa.
Ili kuboresha mazingira bora ya ujifunzaji na ufundishaji shuleni yatakayopelekea kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wanaohitimu masomo ngazi ya Elimu ya Msingi na Sekondari, Serikali imegawa vitabu 6393 Kwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Januari 29,2020 katika Ofisi za Manispaa ya Mtwara kati ya Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Bwana Grayson Orcado na Mwakilishi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Bi. Joyce Shuma.
Katika mgao huo Idara ya Elimu Sekondari imepokea Vitabu 2493 vya kujifunzia (kiada) vitakavyotumiwa na wanafunzi wa Kidato cha kwanza na cha pili kwa masomo ya Historia na Jiografia , na Kidato cha Sita kwa masomo ya Sayansi (Kemia, Fizikia, Biolojia na Hesabu).
Aidha Idara ya Elimu Msingi imepokea Vitabu 3,900 vya kujifunzia kwa wanafunzi wa darasa la sita na vitabu vya kufundishia vya walimu katika masomo ya Kiswahili, Hisabati, Sayansi na Teknolojia, Maarifa ya Jamii, Stadi za kazi, Uraia na Maadili pamoja na somo la kingereza.
Akizungumza wakati wa kupokea Vitabu hivyo Kaimu Mkurugenzi ameishukuru Serikali kwa kuleta vitabu hivyo na kwamba vitasaidia kuondoa changamaoto ya uhaba wa Vitabu katika shule zote hivyo ufundishaji utakuwa rahisi Zaidi.
Aidha ametoa rai kwa wanafunzi na walimu kuvitumia vema vitabu hivo ikiwemo kuvitunza na kuhakikisha kila mmoja anapata fursa ya kujisomea na kufundishia.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.