Kuelekea kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajia kufanyika kwa siku saba kuanzia Januari 12 mwaka huu waandikishaji wasaidizi na “BVR operators” waliochaguliwa na Manispaa ya Mtwara -Mikindani kufanya kazi hiyo wamepatiwa mafunzo yanayolenga kuwawezesha washiriki hao kuelewa jinsi ya kutumia fomu na BVR Kits
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo iliyofanyika Januari 9 katika Ukumbi wa mikutano wa Benjamini Mkapa uliopo Chuo Cha Ualimu Mtwara(TTC) Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko amewataka washiriki kuzingatia maelekezo yatakayotolewa na Tume na kuyafanyia kazi kwa kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa zoezi linafanyika kwa ufanisi mkubwa.
Aidha Mwaigobeko ametoa wito kwa washiriki kuhakikisha wanatunza vifaa vyote vitakavyotumika na kuwataka Mawakala wa vyama vya siasa kutowaingilia watendaji wanapotekeleza wajibu wao .
Mafunzo hayo ambayo yanahusisha ujazaji wa fomu zitakazotumika kwenye zoezi la Uboreshaji wa Daftrai la kudumu la Wapiga Kura na Mafunzo kwa vitendo yanayohusu namna ya kutumia BVR Kits yameanza leo na yatamalizika kesho.
Zoezi la Uboreshaji wa daftrai la kudumu la wapiga kura linatarajia kuanza rasmi Januari 12 na litamalizika Januari 18 mwaka kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara. Aidha jumla ya vituo 118 vya Manispaa ya Mtwara-Mikindani vimeandaliwa kwa ajili ya zoezi hilo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.