Wananchi wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani wametakiwa kuiunga mkono kwa asilimia 100 Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa Serikali imetekeleza vitu vingi kwa vitendo.
Rai hiyo Hiyo imetolewa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu Mzee Mkongea Ali kwenye kila mradi uliopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu ndani ya halmashauri yetu.
Amesema kuwa fedha nyingi zilizotumika katika miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu na ambayo haijapitiwa zimetolewa na Serikali na hivyo kuwataka wananchi kuachana na dhana ya kusema vyuma vimebana .
‘’Kama vyuma vingekuwa vimebana miradi ya maji kama hii tungeipata wapi, Elimu bure bila malipo kabla ya yeye haikuwepo, kuna vituo vya afya visivyopungua 352 nchi nzima na hospitali 67 za Wilaya zimejengwa, Bajeti ya afya imeongezeka kutoka Trilion 1.9 hadi Trilion 2.2”alisema Mkongea
Aidha amempongeza Mkurugenzi na Timu yake kwa utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na kusema kuwa wataalamu wamefanya kazi kw uaminifu na uadilifu mkubwa .
Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe. Anastanzia Wambura amempongeza Rais wa Jamhuri wa Tanzania kwa kutekeleza robo tatu ya Ilani ya Chama hicho kwa kipindi cha miaka 4
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.