Kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani yanayofanyika kila mwaka ifikapo Machi 8 ya kila mwaka, Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali na wadau wa Maendeleo pamoja na wanawake wa Manispaa leo Machi 1,2019 wameshiriki ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Naliendele ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya siku ya wananwake duniani iitakayoyofanyika Machi 8.
Pamoja na ujenzi wa madarasa hayo pia wanawake hao wamejipanga kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuwatembelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo kuwapatia vifaa mbalimbali vya shu;e pamoja na kuwapatia bima za afya watoto zaidi ya 100. Aidha watawatebelea wagonjwa na wajawazito waliopo hospitalini kwa lengo la kuwapa faraja na kuwapatia vifaa mbalimbali vikiwmeo shuka , sabuni na vifaa vingine muhimu.
Akizungumza kweye uzinduzi huo Afisa Utumishi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo bi Tamko Ally amesema kuwa wananwake wameamua kujitolea kujenga madarasa katika shule ili kupunguza mlundikano w awanafunzi darasani uiosababishwa na sera ya elimu bure iliyopelekea kuongezeka kwa idadi ya wannafunzi kwenye shule nyingi.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Naliendele Dionista Kapinga amefarijika sana kwa ujio wa wananwake kutoka sehemu mbalimbali na kushirriki ujenzi w amadrasa katika shule yake kwani imekuwa ni chachu ya maendeleo ya ujenzi wa madarasa hayo.
Siku ya mwannamke duniani inafanyika kila mwaka Duniani ifikapo Machi 8, na kwa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani maadhimisho hayo yatafanyika kwneye viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara yakiongozw ana Mgeni rasmi Mhe Anastanzia Wambura Mbunge viti maalumu
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.