Kutokana na kutoridhisha kwa maendeleo ya usajili na utoaji vyeti kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano,Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Bi. Juliana Manyanya ametoa wito kwa wasajili wasaidizi katika halmashauri hii kwenda kutoa hamasa na elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa usajili wa vyeti vya watoto chini ya Miaka mitano.
“Nendeni mkafanye kazi katika maeneo yenu , hali ya usajili wa yeti vya kuzaliwa bado ipo chini sana, wananchi wanahitaji kuelimishwa wengine hawana uelewa juu ya umuhimu wa vyeti hivi, sasa hivi kila ukienda ofisi mbalimbali wanakuomba cheti cha kuzaliwa, ni muhimu na haki ya kila mtu” Alisema
Ametoa wito huo alipozungumza na wasaidizi hao katika kikao kazi cha kuwajengea uwezo kilichofanyika Juni 20, 2021 katika ukumbi wa Shule ya Msingi St.Michael iliyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Manyama ameendelea kuwashukuru UNICEF kuwa kudhamini mafunzo hayo na kuendelea kuwajengea uwezo wasajili hao.
Baada ya mafunzo hayo wasajili wasaidizi watafanya kampeni ya uandikishaji na utoaji vyeti kwa siku siku nne kuanzia juni 21 hadi juni 214,2021
Aidha RITA imerahisisha uhakiki na usajili wa vyeti vya kuzaliwa, mwananchi anaweza kufanikisha mazoezi hayo kupitia tovuti ya www.rita.go.tz kwa gharama ya shilingi 3000/= kwa uhakiki wa vyeti na 10000/= kwa usajili wa cheti kipya.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.