MKuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka wavuvi Pamoja na wadau wa Uvuvi wanaofanya shughuli zao katika soko la samaki la feri lililopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuendelea kutii sheria ya Uvuvi iliyofanyiwa marekebisho kipengele cha matumizi ya nyavu mtando (ring net) inayowataka wavuvi kutumia vyavu hizo kuvulia samaki wakati wa usiku badala ya mchana kama ilivyokuwa inatumika awali.
Kyobya ametoa rai hiyo Agosti 20,2020 alipokutana na wavuvi hao akiwa kwenye ziara zake za kusikiliza kero za wananchi ambapo alipokea malalamiko ya wavuvi kuhusu sheria hiyo na kuomba Mkuu wa Wilaya kufuatilia Wizara husika waruhusiwe kutumia nyavu hizokuvua hata mchana kwa kuwa bandari ya Mtwara ina kina kirefu kuliko bandari zote nchini hivyo uvuaji wa mchana hautaathiri uharibifu wa mazingira ya bahari.
Pamoja na kutoa rai hiyo Kyobya pia ameahidi kuwasiliana na Wizara husika kuhusu hoja zilizotolewa na wavuvi hao ili kuona zinashughulikiwa vipi kuwasisitiza wafanyabiashara wote waliopo katika soko hilo kukata Vitambulisho vya Wajasiriamali vinavyotolewa kwa Shilingi elfu ishirini tu.
Marekebisho ya sharia ya Uvuvi nchini yameanza kutumika rasmiMwezi Julai mwaka huu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.